BETI NASI UTAJIRIKE

MSHAMBULIAJI WA POLISI TANZANIA AENDELEA KUJIWEKA FITIMshambuliaji wa Polisi Tanzania Marcel Kaheza  amesema kuwa kwa muda huu wa mapumziko ya Ligi Kuu Bara anafanya mazoezi binafsi ili kulinda kipaji chake.

Kaheza ametupia mabao saba na kutoa pasi tano za mabao amekuwa kwenye ubora wake msimu huu ndani ya kikosi hicho akiwa ni kinara wa kutupia mabao.

Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimama kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona. Kaheza amesema kuwa amekuwa akifanya mazoezi ili kulinda kipaji chake pamoja na kuchukua tahadhari ya Virusi vya Corona.

"Ninaendelea kulinda kipaji changu na kufanya mazoezi ili kuwa bora kwani mchezaji lazima afanye mazoezi ili kuzidi kujiimarisha.

"Pia ninachukua tahadhari ya Virusi vya Corona ili kulinda afya yangu pamoja na ndugu ambao wananizunguka," amesema.

Polisi Tanzania ipo nafasi ya sita kwenye msimamo ikiwa na pointi 45 baada ya kucheza mechi 29 za Ligi Kuu Bara.
Marcel Kaheza anayekipiga Polisi Tanzania amefunga mabao saba na ametoa pasi tano za mabao

Post a Comment

0 Comments