BETI NASI UTAJIRIKE

MO DEWJI AMHAKIKISHIA SVEN HATAMFUKUZA KAZI HATA WAKIFUNGWA NA YANGAMwenyekiti wa Bodi ya Ukurugenzi ya Simba SC, Mohamed ‘Mo’ Dewji amempongeza kocha Mkuu wa klabu hiyo, Mbelgiji Sven Ludwig Vandenbroeck kwa kazi nzuri inayoifanya timu ing’are katika soka ya Tanzania. 

“Hongera kocha Sven kwa kazi nzuri. Kwa kweli wachezaji wetu wanajituma kwenye michezo yote tunayocheza. Sasa tujipange kwa mchezo wa jumapili na watani wetu. Lengo letu ni kuwa Mabingwa! Isha’Allah tutafanikiwa,”amesema Dewji kupitia mitandao ya kijamii

.
Pongezi za Mo Dewji zinakuja siku moja tu baada ya mabingwa watetezi, Simba SC kuendelea kudhihirisha ubora wao katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara kufuatia ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Azam FC usiku wa jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 


Ushindi huo, Simba SC ifikishe pointi 68 baada ya kucheza mechi 26, sasa ikiizidi pointi 20 Azam FC inayofuatia nafasi ya pili – na wakati huo huo Wekundu wa Msimbazi wametinga Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC). 

Kwa upande mwingine kauli ya Mo Dewji inaonyesha ni kiu yake ya ubingwa kwa msimu wa tatu mfululizo na hata Simba ikifungwa na watani zao Yanga basi Sven ataendelea kuwa kocha w klabu hiyo.

Baada ya ushindi wa juzi Simba SC ilirejea kambini kujiandaa na mchezo mwingine mgumu wa Ligi Kuu dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Yanga Jumapili hapo hapo Uwanja wa Taifa.

Post a Comment

0 Comments