BETI NASI UTAJIRIKE

WAWA APEWA MAJUKUMU MAZITO ,AJIPANGA KUMPOTEZA MORISSON


Mlinzi wa kati wa Simba, Pascal Wawa raia wa Ivory Coast amefunguka kuwa amemfuatilia vizuri kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mghana, Benard Morrison na kukiri kwamba ni mchezaji mzuri lakini katika mchezo wa leo Jumapili mashabiki wa timu yake watamsahau kabisa.

Wawa ametoa kauli hiyo kuelekea katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara unaotarajia kupigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar

Wawa ndiye mhimili wa eneo la ulinzi la Simba na Morrison amekuwa akitegemewa zaidi katika kufunga na kutengeneza nafasi kwa upande wa Yanga

Wawa amesema mchezo huo hautakuwa rahisi kama watu wanavyotegemea kutokana utamaduni ya mechi hizo lakini akaapia kuwa Morrison atasahaulika kabisa kwa namna atakavyomdhibiti.

"Naamini mchezo kwanza hautokuwa wa kawaida kwa sababu naelewa juu ya timu hizi zinapokuwa zinakutana kutokana na muda ambao nipo hapa kwa sababu asili ya mechi yenyewe na hamasa inakuwa kubwa kabla ya mchezo lakini kwa upande wetu tumejipanga kushinda ili kuongeza nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa msimu huu.

"Morrison ni mchezaji mzuri nimejaribu kumuangalia kidogo, nimeona ubora wake hilo siwezi kukataa lakini naamini hizi timu zinapokutana kila mtu anajua kinachotokea na kwangu hii ni changamoto ambayo nimejipanga kuizima mapema kiasi cha mashabiki wa timu yake washindwe kuona ubora wake kutokana na mipango iliyopo," alitamba Wawa.

Post a Comment

0 Comments