BETI NASI UTAJIRIKE

MANCHESTER UNITED KUWAKOSA BAADHI YA NYOTA WAKE MECHI DHIDI YA MANCHESTER CITY
Hapo kesho nyasi za Old Trafford zitawaka moto kwani wapinzani wa jadi Manchester United wataikaribisha Manchester City kwenye mchezo wa ligi kuu England. Manchester United wana point 42 wakiwa nafasi ya 5 na watatakiwa kushinda mchezo huo ili waweze kupanda mpaka nafasi ya 4 huku Manchester City wanatakiwa wapambane zaidi kuelekea mbio za ubingwa wakiwa na pointi 57 huku Liverpool anayeongoza akiwa na pointi 79.

Msimu huu Manchester United imekutana na City kwenye michezo mitatu huku ikishinda michezo 2 na kupoteza mmoja na huu utakuwa ni mchezo wa nne kwa msimu mmoja kuweza kukutana.


Kikosi cha Manchester United kimeendelea na mazoezi katika viunga vya Carrington huku kukiwa na wasiwasi wa kukosekana kwa beki Maguire,Daniel James  na, Wan bissaka kwenye mchezo huo.Marcos Rashford na Paul Pogba wataendelea kukosekana kwenye mchezo huo kutokana na majeraha . Kocha wa klabu hiyo amenukuliwa akisema 

"Nina imani Wan Bissaka na Daniel James watakuwepo kwenyemchezo huo ingawa hakuna hata mmoja kati yao aliyefanikiwa kufanya mazoezi na timu mara baada ya mchezo na Derby Contry hivyo tutaangalia uwezo wao siku ya jumamosi"

Manchester United imejikuta kwenye wakati mzuri tangu Ighalo na Bruno Fernandez wakiisaidia timu hiyo kutopoteza michezo 6 mfululizo. Hizi ni baadhi ya picha za wachezaji wa Manchester United wakiwasili mazoezini.


Post a Comment

0 Comments