BETI NASI UTAJIRIKE

MANARA:NIPO TAYARI KUACHA KAZI SIMBA NA KWENDA KUFUNDISHA MADRASAMsemaji wa Simba ameendelea kuwakera mashabiki wa Yanga baada ya kusema yupo tayari kuacha kazi na kwenda kufundisha Madrasa endapo tu klabu yake ya Simba itamtaka apige promo mechi yao na Yanga kwa kutumia magari badala ya vyombo vya habari. 

Manara ameandika kauli hiyo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii huku akiambatanisha picha ya gari la matangazo litumikalo kuuza jezi na kupromote mechi kati ya Yanga na klabu ya Simba itakayopigwa siku ya jumapili. 

Kauli hiyo ni mwendelezo wa majibizano kati yake Jerry Muro aliyemtaka aache kazi ya usemaji ndani ya Simba na arejee kufundisha madrasa kwani ni elimu pekee aliyonayo. Manara ameandika hivi

Ukubwa wa Simba hauwezi kuturuhusu Game zetu kufanyiwa Promo kama tangazo la Condom au Taarab,,Simba haihitaji hz Promo za kilevi,,hv vtu tuwaachie wauza vocha za jero jero Guys!!ðŸĪŠ siku viongozi wangu wakiniambia Haji fanya promo kama hz ktk idara yangu narudi Madrasa kufundisha,,mm ni mkubwa sana kufanya vtu kama hv 😄😅


Post a Comment

0 Comments