BETI NASI UTAJIRIKE

NUGAZ ALIVYOMCHAMBUA FEISAL SALUM "FEI TOTO"



Mabadiliko ya soka duniani yameleta vitu vingi sana, Advanced playmaker, deep lying na Box to box midfielder, nchini Tanzania nimeanza kushuhudia hivi punde Makocha wakianza kucheza na mbinu mpya kiufundi

Mtoto mmoja kutoka visiwa vya Karafuu pale Zanzibar kwenye ubuyu wa Babu Issa, wakuitwa Feisal Salum ndie mtu wa kwanza kushangaza watu

Zahera anampangaje Feisal chini?? Lile sio eneo lake bwana, yule anatakiwa acheze nyuma ya Mshambuliaji! Maneno ya Waswahili na wanafasihi huko mtaani
Wakati wakina Ancelotti, Mazzone na Michael Zagallo wanatupikia kiungo mpya ni wazi waliamini ni ngumu kueleweka ila Luc Eymel na Charles Mkwasa wanatukumbusha tena mawazo ya mafundi wale wa zamani juu ya Regista role au Meia Armado

Feisal anakaa chini kama Andrea Pirlo, kazi yake haipaswi kuwa kukaba sana, huyu ndie anatengeneza umbo la mashambulizi ya timu na mchezo (deep lying playmaker) anapiga pass fupi na ndefu, huyu pia ana uwezo wa kupiga mashuti nje ya box
Kumbuka msimu uliopita alitia kamba ngapi nje ya box ili Feisal awe bora lazima pembeni yake kuwe na mtu wa kufanya kazi zote chafu, hapa una mapafu kama ya Captain Pappy Tshishimbi au Makame Bui, anakaba, anatia kwanja na kumlainishia njia ya kupitia fundi wa mpira
Ndicho kinafanyika kwa Wananchi, wamebadilika na kuja na mfumo huu baada ya kugundua kuwa timu nyingi zikicheza offside trick, wakaona isiwe tabu tutoke kwenye mita 40 tucheze kwenye mita 70 chini kabisa
Ni mfumo rafiki huu na ni mwepesi kueleweka kichwani mwa Fei Toto
Uhuru wa Feisal eneo hilo unabebwa na ubora wa kimbinu, beki nne za nyuma kuna muda wanacheza kama narrow backfour, kisha mawinga wanakuja chini, hapo Feisal anafanya anachotaka, anapiga pass za kusambaza upendo, anagawa kadi za harusi na biriani kwa mastraika kufanya watakacho Wananchi
Kwenye transition lazima wapite kwa Fei Toto ndie akili ya Yanga, ndie kiwanda cha maarifa, ataamua muda gani timu ikae, muda gani itoke na wapinzani wapo sehemu gani na apige pass gani
Wape salamu na uwaambie Chuma kipo Zanzibar kinajifua binafsi...!

Post a Comment

0 Comments