BETI NASI UTAJIRIKE

LIVERPOOL YAPIGWA TENA , MECHI MBILI WAPIGA SHUTI MOJA TU GOLINI

Klabu ya Liverpool imemaliza mwezi wa pili kwa staili ya aina yake baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya Watford. Awali Liverpool ilikuwa imecheza michezo 19 bila kupoteza pointi yeyote.Hiyo inakuwa mechi ya pili mfululizo kwa Liverpool kufungwa ndani ya wiki moja huku safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Sadio Mane,Firmino na Mohammed Salah kuonekana butu baada ya kucheza mechi mbili na kupiga shuti moja tu lililolenga golini.

Magoli ya Watford yalifungwa na Ismael Sarr dakika ya 54,60 na Troy deeney dakika ya 72. Matokeo hayo yanawafanya Watford kufikisha pointi 27 kwenye michezo 28 waliyocheza na kupanda mpaka nafasi ya 17 kwenye msimamo wa ligi

Liverpool ilipokea kipigo cha kwanza kutoka kwa Atletico Madrid kwenye mchezo wa ligi ya  mabingwa ulaya huku wakishindwa kupiga shuti hata moja lililolenga golini. 

Kwa upande wa msimamo wa ligi bado wanaongoza ligi wakiwa na pointi 79 kwenye michezo 28 waliyocheza huku wakishinda michezo 26 ,sare 1 na kufungwa 1. Kama ligi haita ahirishwa msimu huu kutokana na hofu ya Corona barani ulaya basi Liverpool wataweza kutwaa kombe hilo kwa staili ya aina yake msimu huu.


Post a Comment

0 Comments