BETI NASI UTAJIRIKE

KOCHA EYMAEL WA YANGA AITWA NA UONGOZI


Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael anatarajiwa kukutana na uongozi wa timu hiyo kujadili masuala mbalimbali yanayowahusu wachezaji hasa matukio ya utovu wa nidhamu
Hivi karibuni Eymael alitoa malalamiko kwa uongozi akiwashukia baadhi ya wachezaji ambao hawakusafiri na timu mkoani Lindi kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc ambao ulipigwa juzi kwenye uwanja wa Majaliwa, Ruangwa

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amethibitisha kuwepo kwa kikao hicho ambacho maamuzi yake yanaweza kuwaweka matatani baadhi ya nyota

"Tumemsikia Mwalimu akitoa malalamiko yake kuhusu baadhi ya wachezaji lakini leo atapata nafasi ya kukaa na uongozi kujadili masuala hayo kwa kina. Lakini mwisho wa siku ni yeye mwenyewe atakayekuwa na maamuzi ya mwisho kuhusu hatua ambazo zitapaswa kuchukuliwa," amesema Bumbuli

Taarifa zilizopatikana mapema leo zilibainisha kuwa tayari mshambuliaji Mcongomani David Molinga amepewa siku tatu ajieleze kwa nini asiadhibiwe baada ya kukosa safari ya Lindi

Post a Comment

0 Comments