BETI NASI UTAJIRIKE

HIVI NDIVYO MKUDE ALIVYOPONEA CHUPU CHUPU KUIKOSA YANGA


Kiungo wa Simba, Jonas Mkude na straika wa Yanga, Bernard Morrison, hawatajadiliwa na Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) hadi baada ya mechi ya ‘mabosi’ hao wa soka nchini itakapochezwa Jumapili wiki hii.

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi iliwachongea Mkude na Morrisons kwenye Kamati ya Maadili baada ya kukutwa na hatia ya kuwachapa viwiko wachezaji wenzao katika mechi tofauti.

Kiungo Mkude alimpiga kiwiko mchezaji wa Biashara United, Ally Kombo katika mchezo wa ushindi wa mabao 3-1 walioupata Simba kwenye Uwanja wa Taifa.
Morrison naye alifanya hivyo hivyo kwa Jeremiah Juma wa Prisons katika mechi ya sare ya bila kufungana. Kwa mujibu wa kanuni za ligi za TFF, wawili watalazimika kukaa ‘benchi’ michezo mitatu kama makosa yao yatathibitishwa.

Hata hivyo, kutokuhojiwa kwako na kamati ina maana wanaweza kukipiga katika mechi ya watani wa jadi wiki hii.

Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu Wakili, Kiomoni Kibamba, amesema ilikuwa wakutane Jumapili iliyopita, lakini walishindwa kutokana na ratiba za wajumbe kutokuwa rafiki kuwawezesha kukutana.

"Ili kamati isikilize kesi, lazima idadi itimie au kuwa nusu yake, lakini kutokana na majikumbu mbalimbali kamati haikuweza kukutana," Kibamba amenukuliwa

'Mwisho wa wiki hii, wajumbe wengi wa kamati ya nidhamu tutakuwa Dar es Salaam, hivyo tutakutana na kupitia kesi zote zilizoletwa mezani," alisema Kibamba. Aliongeza: "Bila shaka hadi itakapofika Jumatatu ijayo, masuala yote tutayamaliza."

Post a Comment

0 Comments