BETI NASI UTAJIRIKE

SIBOMANA ATANGAZA HALI YA HATARI KWA ATAKAYECHEZA NA YANGA


Kiungo mshambuliaji wa Yanga Patrick Sibomana amesema kuwa ataendelea kupachika mabao kila atakapopewa nafasi na kocha Luc Eymael.Baada ya kukosekana kwa wiki kadhaa, Sibomana jana alirejeshwa kwenye kikosi cha kwanza katika mchezo dhidi ya Mbao Fc ambapo alifunga bao la pili na kuihakikishia Yanga ushindi wa mabao 2-0
Hilo lilikuwa bao lake la tano msimu huu

Akizungumza baada ya mchezo huo, Sibomana alisema lilikuwa jambo la faraja kwake kurejea kikosini na kufanikiwa kuifungia Yanga
Aidha nyota huyo kutoka Rwanda amesema amejiwekea malengo ya kufunga angalau mabao 10 msimu huu

"Kuifungia timu mabao ni jukumu langu, hivyo nitahakikisha nafunga kila nitakapopewa nafasi ya kucheza. Kwa msimu huu nimejiwekea malengo ya kufunga mabao 10 au zaidi. Bado mechi zipo nyingi, malengo hayo naweza kuyatimiza
Kuhusu nafasi ya kucheza ni jukumu la mwalimu kupanga nani acheze, muhimu nitahakikisha nafanya vizuri ili niendelee kupewa nafasi ya kucheza," alisema Sibomana

Tangu kutua kwa Eymael, Sibomana amepoteza nafasi kwenye kikosi cha kwanza lakini pia ujio wa Bernard Morrison umechangia
Morrison amekuwa akifanya vizuri winga ya kushoto ambayo mara nyingi Sibomana hucheza

Post a Comment

0 Comments