Kiungo mshambuliaji wa Yanga Bernard Morrison leo amekabidhi mkataba aliosaini ambao utamuweka Jangwani kwa miaka miwili zaidi
Klabu ya Simba ilikuwa ikimnyemelea mshambuliaji huyo lakini sasa ni rasmi hawawezi kumpata baada ya kusaini mkataba mpya
Taarifa iliyotolewa na Yanga mapema leo imethibitisha kuwa Morrison amesaini mkataba wa miaka miwili
"Mshambuliaji wetu Benard Morrison leo amerejesha Mkataba wake aliosaini ili kuendelea kuitumikia Klabu yetu ya Yanga kwa kipindi cha miaka miwil"
"Shukran kwa wadhamini wetu chapa GSM kupitia Mkurugenzi wa uwekezaji Eng. Hersi Said"
Inasemekana mkataba huo utamfanya Morrison kuwa ni mchezaji anayeingiza fedha nyingi ndani ya Yanga na anakuwa mchezaji anayelipwa zaidi kwa wachezaji wote wanaoshiriki ligi kuu
Taarifa nyingine zinasema ili kuuvunja mkataba wa Morrison Klabu yoyote itatakiwa kulipa milioni 500 za kuvunja mkataba na milioni 500 ada ya usajili na kumfanya awe mchezaji ghali zaidi ligi kuu akiwa na thamani ya bilioni 1

0 Comments