BETI NASI UTAJIRIKE

DAVID MOLINGA "FALCAO" KUIKABILI MBAO FC LEO


Kinara wa mabao kikosi cha Yanga David Molinga huenda akarejea kikosini leo Jumanne kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbao Fc.Mchezo huo utapigwa kwenye uwanja wa Taifa, saa moja jioni

Molinga alikosekana kikosini katika mechi za hivi karibuni akiruhusiwa kurejea nyumbani kwake Ufaransa kushughulikia matatizo binafsi.Nyota huyo alirejea tangu wiki iliyopita hata hivyo kocha Luc Eymael hakumtumia katika mechi zilizopita kwa kuwa hakuwa fit

Molinga amefunga mabao saba kwenye ligi. Ndiye anayeongoza miongoni mwa wachezaji wa Yanga.Ditram Nchimbi amefunga mabao sita, manne akiyafunga wakati yuko Polisi Tanzania

Patrick Sibomana amefunga mabao manne, naye hakuwepo kikosini kwa wiki kadhaa baada ya kuruhusiwa kurejea Rwanda kuhuisha VISA ya mkeweS.Sibomananae anaweza kuonekana dimbani kwenye mchezo wa kesho

Post a Comment

0 Comments