BETI NASI UTAJIRIKE

KAPOMBE : TULETEENI HAO YANGA TUMALIZE KAZI


Beki wa kulia wa Simba Shomari Kapombe amesema baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Azam Fc, sasa wanaelekeza nguvu zao kuelekea mchezo wa Yanga Jumapili
Kapombe alitengeneza bao la ushindi la Simba jana kwa kumimina majaro murua iliyotua mguu kwa Meddie Kagere 'MK14' na kuiandikia Simba bao la tatu
"Ulikuwa mchezo mgumu lakini tunamshukuru Mungu tumeweza kuondoka na alama zote tatu. Sasa tunahamishia nguvu zetu kwenye mchezo unaofuata dhidi ya Yanga.."
"Kwetu huu ni mchezo wa kawaida kama ilivyo michezo mingine lakini tutachohitaji ni sapoti ya mashabiki, tunawaomba wajitokeze kwa wingi hiyo Jumapili," alisema Kapombe

Kapombe aliongea kwa kujiamini kuelekea Mchezo huo na ameonyesha dhahiri watapata ushindi kwenye mchezo huo.

Agoma kurejea timu ya Taifa
Katika hatua nyingine, Kapombe amesema bado msimamo wake wa kun'gatuka kuichezea timu ya Taifa haujanbadilika
Baada ya kupona majeraha, kiwango cha Kapombe kimeimarika na wengi walipenda kumuona akijumuishwa kwenye kikosi cha Stars ambacho kitashiriki michuano ya CHAN mwezi ujao huko Cameroon
Kapombe amesema wakati wa kurejea timu ya Taifa bado haujafika

Post a Comment

0 Comments