BETI NASI UTAJIRIKE

JOSIP ILICIC APIGA NNE PEKE YAKE , TOTTENHAM YA MOURINHO HAMNA KITU


Klabu ya Tottenham imeondolewa kweye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya akuruhusu kipigo cha mabao 3-0 ugenini dhidi ya RB Leipzig. Magoli ya RB. Leipzig yalifungwa na Marcel Sabtizer dakika ya 10 na 21 huku lile la  tatu likifungwa na Emil. 

Tottenham imekuwa timu ya kwanza kutolewa michuano ya UEFA kwa msimu huu ikikubali kutolewa kwa jumla ya mabao 4-0. 


Kwa upande mwingine klabu kutoka Italy Atalanta imeonyesha ubabe baada ya kuwaondoa Valencia kwa jumla ya mabao 8-4. Mchezo wa kwanza Atalanta waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 huku mchezo wa jana usiku wakiibuka na ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya wababe hao wa hispania .


Mabao ya Valencia yalifungwa na Kelvin Gameiro dakika ya 21 na 51 huku Ferran Torres akifunga dakika ya 67. Mabao manne ya  Atalanta yalifungwa na Josep LLicic  na kuifanya timu hiyo kufuzu hatua ya robo fainali.


Post a Comment

0 Comments