Nyota 11 ndani ya kikosi cha Yanga inaelezwa kuwa mikataba yao inafika ukingoni mwishoni mwa msimu huu huku panga likiaandaliwa kupita nao jumlajumla. Habari kutoka ndani zinaeleza kuwa miongoni mwa makosa ambayo kamati ya usajili ilifanya ni kusajili nyota wengi ambao hawana mchango mkubwa jambo ambalo linafanyiwa kazi kwa sasa. "Kamati ya usajili iliongeza nyota wengi ambao hawakufanyiwa mchakato mzuri wa kuwatazama ndio maana wamekuwa na mchango mdogo, ila kwa sasa makosa hayatarudiwa na baadhi ya nyota wataondolewa," kilieleza chanzo hicho. Miongoni mwa nyota ambao mikataba yao inakaribia kumeguka ni Kelvin Yondan, Andrew Vincent, Said Juma Makapu, Ramadhan Kabwili, Feisal Salum, Mohammed Issa, David Molinga, Jaffay Mohamed, Ally Ally, Yikpe Gnamien na Eric Kabamba. Inaelezwa kuwa beki, Ally Ally mwenye pasi moja ya bao ndani ya Yanga hana maisha marefu ndani ya kikosi hicho huku Kabamba, Molinga, Yikpe wakitazamwa kwa ukaribu kabla ya panga kuwapitia.
0 Comments