Ushindi wa mabao 5-0 walioupata Manchester United mbele ya LASK kwenye mchezo wa Europa League unamfanya nyota wao mpya Odion Ighalo afikishe jumla ya mabao manne tangu atue kikosini hapo.
Ighalo alijiunga na United kwa mkopo akitokea Klabu ya Shanghai Shenhua ya nchini China kwa mkopo.
Kuliibuka maswali mengi kwa wadau wa soka kuuliza kwa nini United imeamua kumpa dili nyota huyo raia wa Nigeria mwenye umri wa miaka 30 jambo ambalo limeanza kujibiwa taratibu.
Kocha Mkuu Manchester United, Ole Gunnar Solksjaer amesema kuwa anafurahia kumuona Ighalo akiwa ndani ya Uwanja ana amini atafanya mambo mengi makubwa kwa ajili ya timu.
0 Comments