BETI NASI UTAJIRIKE

HII HAPA ORODHA YA WACHEZAJI GHALI ZAIDI WALIOZALIWA BAADA YA MWAKA 2000


Wachezaji wawili wa klabu ya Borussia Dortmund wanaongoza orodha ya wachezaji watano wa soka waliozaliwa baada ya mwaka 2000 walio na thamani ya juu kulingana na shirika la wachunguzaji wa viwango vya soka CIES.
Wachezaji hao wametajwa kuwa Jadon Sancho wa England na Erling Haland wa Norway.Mchezaji wa Uingereza Jadaon Sancho ana thamani ya €200m huku raia wa Norway Erling Haland akigharimu €101m.
Huku thamani ya Sancho ikidaiwa kufikia kilele chake , ile ya Haland inatarajiwa kupanda zaidi.
Haki miliki ya pichaWachezaji hamsini bora wenye thamani ya juu wameorodheshwa katika jarida la Weekely Post.
Katika nafasi ya tatu ni raia mwengine wa Ujerumani anayechezea ligi ya Bundesliga Alphonse Davies mwenye thamani ya €92m.
Washambuliaji wawili wa Real Madrid Rodrygo na Vinícius ambao wanaorodheshwa katika nafasi ya nne na ya tano wamedaiwa kuwa na thamani ya €89m na €74m mtawalia.
Ikiwa na wachezaji wanne walioorodheshwa katika orodha hiyo England ndio nchi iliowakilishwa zaidi katika wachezaji 10 bora.
Washambuliaji wawili wa Real Madrid Rodrygo na ViníciusHaki miliki ya picha
Taifa hilo linawakilishwa na Jadon Sancho, Callum Hudson-Odoi akiwa katika nafasi ya 6, na thamani ya €72m, naye Mason Greenwood anashikilia nafasi ya 9 akiwa na thamani ya €50m na hatimaye Phil Foden anayefunga kumi bora akiwa na thamani ya €50 M.
Akiwa na thamani ya €53m, kiungo wa kati wa Ufaransa Eduardo Camavinga anayeichezea klabu ya Stade Rennais ndio mchezaji mwenye umri mdogo zaidi katika orodha ya kumi bora.
Mchezaji mwengine aliyezaliwa 2002, Ansu Fati anayeichezea klabu ya FC Barcelona ana thamani ya €40m.
Ansu fati
Ripoti hiyo ya mwezi wa 53 inatoa mifano na njia iliyofuatwa na shirika la wachunguzaji wa soka CIES ili kutathmini viwango vya uhamishaji vya wachezaji soka katika misingi ya kisayansi.

Post a Comment

0 Comments