BETI NASI UTAJIRIKE

HARUNA NIYONZIMA ATUMA SALAMU ZA VITISHO KWA NAMUNGO FC


Kiungo fundi wa Yanga Haruna Niyonzima 'Fabregas' amesema watauchukulia kwa uzito mkubwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa keshokutwa Jumapili kwenye uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi, Wilaya ya Ruangwa

Niyonzima amesema matokeo ya kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa KMC hawakuyatarajia kwani walijiandaa kushinda mchezo huo lakini wapinzani wao wakawaotea
Amesema mchezo dhidi ya Namungo Fc wanahitaji kushinda ili kurejesha furaha ya mashabiki wao

"Namungo ni timu yenye ushindani ndio maana ipo nafasi ya nne, hivyo tunajua tutakuwa na kazi ngumu kwenye huo mchezo ingawa naamini tutashinda," alisema Niyonzima jana baada ya mchezo dhidi ya KMC
"Unajua sisi wachezaji hatuwezi kuridhika na kuifunga Simba kwamba ndio tumemaliza kila kitu bado tunahitaji kuwatengenezea mashabiki wetu furaha na kuipa heshima Yanga, hivyo imetokea bahati mbaya KMC wametuotea na sasa hatukubali kwa Namungo"

Yanga iko nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 50 wakati Namungo Fc ina alama 49 ikiwa nafasi ya nne.Namungo pia wamecheza mchezo mmoja zaidi ya Yanga

Post a Comment

0 Comments