BETI NASI UTAJIRIKE

FUNDI ALIYECHEZA NA MORRISON PALE ORLANDO KUTUA SIMBA



Justin Shonga ni raia wa Zambia anayekipiga ndani ya Klabu ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini.Amezaliwa Novemba 5,1996 ana umri wa miaka 23 kwa sasa akiwa na urefu wa m 1.79 na uzito wa kg 65.

Inaelezwa kuwa Klabu ya Simba ipo kwenye hesabu za kuinasa saini ya nyota huyo ambaye dau lake inaelezwa ni milioni 800.

Alijiunga na Orlando Pirates 2017 akitokea Klabu ya Nkwazi FC ya Zambia, pia anakipiga ndani ya timu ya Taifa ya Zambia kwa nafasi ya ushambuliaji.

Kwa ujumla tangu 2017 mpaka sasa amecheza mechi 24 na timu ya Taifa ambapo amefunga mabao
13.

Post a Comment

0 Comments