Ukweli ni kwamba msimu huu unaelekea ukingoni na Yanga haiwezi kufikia malengo yake ya kutwaa ubingwa ambayo yaliwekwa mwanzoni mwa msimu.Mabadiliko ya kikosi na benchi la ufundi, inaweza kuwa sababu ya kuifanya Yanga isiwe na mwendelezo mzuri
Tangu mwezi Juni mwaka jana, Yanga imesajili wachezaji 22 na kubadilisha benchi la ufundi mara tatu
Sasa ili kuhakikisha msimu ujao timu inakuwa imara, uongozi wa Yanga kwa kushirikiana na wadhamini wao GSM, wamempa kocha Luc Eymael ruhusa ya kuanza kusaka wachezaji anaotaka wasajiliwe
Kocha huyo ametakiwa kuangalia maeneo yenye mapungufu na sio kusajili timu nzima na bila mpango kama ilivyokuwa kwa Mwinyi Zahera.Moja ya maeneo ambayo wanayanga watarajie kuona mabadiliko ni safu ya ushambuliaji
Washambuliaji David Molinga na Yikpe Gnamien wana uwezekano mdogo wa kuendelea kuwa sehemu ya kikosi cha Yanga msimu ujao.Molinga alisajiliwa kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea Renaissance, anatarajiwa kurejea kwenye klabu hiyo inayoshika nafasi ya tano Ligi Kuu ya DRC
Kwa Gnamien mabosi wa Yanga watalazimika kuvunja mkataba wake kwani alisaini miaka miwili.Eymael ameahidi kuwa ataleta washambuliaji ambao wataifanya safu ya ushambuliaji iwe moto wa kuotea mbali msimu ujao
Amesema anawafahamu wachezaji wazuri ambao watain'garisha safu hiyo kwa kushirikiana na Bernard Morrison na washambuliaji wazawa
Usajili wa Morrison ni pendekezo la Eymael Yanga ikimnasa Januari 15, siku ambayo dirisha dogo la usajili lilifungwa.Habari njema ni kuwa Yanga inakaribia kubadili mfumo wake wa uendeshaji na pengine msimu ujao itakuwa mikononi mwa wawekezaji hivyo suala la kusajili wachezaji wakali halitakuwa tatizo kwani fedha itakuwepo.Kuna uwezekano mkubwa GSM wakajitosa 'mazima' kuwekeza Yanga
0 Comments