BETI NASI UTAJIRIKE

DKT.MSOLLA AONGOZA KIKAO CHA DHARULA YANGAUongozi wa Yanga ukiongozwa na Mwenyekiti Dk Mshindo Msolla wamekutana kwa dharura kujadili sintofahamu iliyojitokeza baada ya GSM kutangaza kusitisha baadhi ya huduma kwa klabu hiyo

Kikao hicho ambacho pia kilimshirikisha aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa, Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Walemavu Mh Anthony Mavunde kimemaliza sintofahamu iliyojitokeza

Inaelezwa GSM wamepewa baraka zote kuendelea na majukumu waliyokuwa wakifanya ambapo Dk Msolla amewahakikishia kuwa uongozi wake utaendelea kuwaunga mkono na kushirikiana nao bega kwa bega

Ni jambo jema kuona viongozi wamechukua hatua haraka kumaliza sintofahamu hiyo ambayo tayari ilikuwa imeibua taharuki miongoni mwa wapenzi, mashabiki na Wanachama wa Yanga

Post a Comment

0 Comments