DITRAM Nchimbi, mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa Kocha Mkuu Luc Eymael alimwambia kuwa akatumie makosa ya wapinzani ili akaifungie timu yake mabao.
Jana, Februari 29, Yanga ilishinda mbele ya Alliance mabao 2-0 na kuifanya ifikishe pointi 44 ikiwa nafasi ya nne kwenye msimamo.Mabao yote ya Yanga yaliwekwa kimiani na Super Sub Ditram Nchimbi aliyesajiliwa Dirisha dogo akitokea Polisi Tanzania
Nchimbi amesema:"Mwalimu aliniambia kwamba ninapaswa nitazame mapungufu ya wenzangu na nikafunge ili kuipa timu ushindi na mwisho wa siku ndicho kilichotokea,".
Yanga imeipiga nje ndani Alliance kwani mchezo wa kwanza uliochezwa CCM Kirumba ilishinda kwa mabao 2-1 na jana imeshinda mabao 2-0.
0 Comments