BETI NASI UTAJIRIKE

TATHMINI FUPI MECHI YA SIMBA NA YANGA HAPO KESHO




Derby ya pili  mwaka huu 2020 watani wa jadi  Yanga na Simba ambao utapigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Mchezo huo utakuwa wa  mzunguko wa pili baada ya ule wa awali wa 2-2 kuchezwa  Januari 4, mwaka huu jijini hapa.Hakika utakuwa ni mchezo wenye ushindani kwa pande zote mbili huku kila kocha au klabu itataka kuweka rekodi katika mchezo huo.

 Imani kubwa ya wengi ni kwamba mchezo huo utakuwa kwenye ubora na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili zikihitaji kuweka rekodi mpya.Timu hizo zote zinaamini kuwa zitaibuka na ushindi katika mchezo huo, lakini Yanga na Simba zinatakiwa kuelewa na kutambua kuwa  soka ina matokeo ya aina tatu kushinda, kufungwa na kutoa sare.

  Hivyo kwa maana hiyo timu zinatakiwa kujiandaa kisaikolojia kwa aina yoyote ya matokeo ambayo watapata katika mchezo huo na kuyakubali na si kwa kuanza kuharibu vitu au kuleta fujo za aina yoyote.

Kwa mashabiki pamoja na timu kwa ujumla ni watu ambao wanatambua matokeo ya soka yapo ya aina zote hivyo wawe tayari kwa lolote kwani mechi hiyo ni kama zilivyo mechi nyingine za ligi.Timu yenye nafasi ya kushinda ni ile ambayo imejiaandaa vema kwa kufuata kanuni za soka zinavyotaka.

Kwa maerafa ambao watasimamia mchezo huo wa kesho rai yangu ni kuona kwamba taratibu zinafuatwa na kanuni hazipindishwi.Yale masuala ya malalamiko kwa waamuzi hayapaswi yapewe nafasi kwani presha ya mashabiki ipo siku zote lakini haiwezi kuleta presha kwenye maamuzi ya refa.

Kanuni zipo wazi kuanzia kwa mshika kibendera mpaka refa wa kati ni lazima wakubali kwamba mchezo huo ni sawa na mechi nyingine wasichezeshe kwa mazoea bali umakini unahitajika.

Post a Comment

0 Comments