BETI NASI UTAJIRIKE

CORONA YATIKISA BUNDESLIGA



Chama cha soka Ujerumani kimesimaisha rasmi ligi kuu (BUNDESLIGA) nchini humo kutokana na hofu ya Corona. Ujerumani inaungana na Uhispania,Uingereza,Italia na Ufaransa kusimamisha ligi za ndani. 

Taarifa za awali zinasema ligi hiyo itaendelea kuanzia April 2 kama hali itakuwa shwari duniani kote lakini pia upo uwezekano wa kuitisha mkutano mkuu wiki chache zijazo ili kuzungumizia muendelezo wa ligi hiyo inayoshirikisha timu 18.

Mpaka sasa nchini Ujerumani kuna visa 7,588 huku pia kukiwa na  vifo 17 na waliopona ni 67 pekee.  Kuna uwezekano ligi hiyo isiweze kurejea mpaka mwezi mei kutokana na hofu hiyo ya Corona

Post a Comment

0 Comments