BETI NASI UTAJIRIKE

CECAFA YAPATA MKURUGENZI MPYA NA AAHIDI KUFANYA MAKUBWAMkurugenzi Mtendaji wa CECAFA, Auka Gecheo amesema kuwa atafanya kazi yake hiyo mpya kwa ushirikiano mkubwa na viongozi aliowakuta ili kutimiza malengo waliyojiwekea.

Geucho raia wa Kenya ameteuliwa kuchukua mikoba ya Nicolas Musinye aliyekuwa Katibu Mkuu wa CECAFA aliyedumu kwa miaka 21 katika nafasi hiyo.

Akizungumza na Saleh Jembe, Auka amesema kuwa ni kazi kubwa aliyopewa na ana imani ya kutumika vema kutokana na uzoefu alionao.

"nina uzoefu kwenye masuala ya soka kwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na Rais wa Cecafa Wallace Karia amenipa ahadi ya kunipa ushirikiano nina imani nitafanya kazi kwa ukaribu na kila kiongozi ili kufikia malengo yetu," amesema.

Post a Comment

0 Comments