BETI NASI UTAJIRIKE

DEO KANDA NJIA PANDA KURUDI TP MAZEMBE AMA KUBAKI SIMBAKlabu ya Simba  inamshawishi winga Deo Kanda asaini mkataba wa kudumu kunako mabingwa hao wa nchi.Baada ya kujihakikishia kutwaa ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa tatu mfululizo, mipango iliyopo ni kujenga kikosi imara ambacho kitatoa ushindani kwenye michuano ya ligi ya mabingwa

Kanda ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa wa michuano hiyo, alitua Simba kwa mkopo wa mwaka mmoja ambao unamalizika mwezi Juni.Mcongomani huyo ameonyesha kuwa tayari kubaki Simba hata hivyo klabu ya TP Mazembe ambayo inammiliki nyota huyo mpaka Juni mkataba wake utakapomalizika, nayo inapambana kumrejesha DRC

Kutimuliwa kwa kocha Mihayo Kazembe kunaweza kumshawishi Kanda kusaini mkataba mwingine na mabingwa hao wa DRC.Inaelezwa Kanda hakuwa na maelewano mazuri na Kazembe na ndio sababu iliyofanya nyota huyo alazimishe kuondoka

Baada ya kutolewa hatua ya robo fainali michuano ya ligi ya mabingwa, TP Mazembe ilimsimamisha Kazembe na inaelezwa hatarejea kuendelea kuinoa timu hiyo.Hata hivyo pamoja na mazingira hayo, Simba ina nafasi nzuri ya kumnasa Kanda ambaye amefunga mabao sita kwenye ligi msimu huu

Post a Comment

0 Comments