BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA WAJA NA MFUMO MPYA WA UENDESHAJI, GSM NA ROSTAM WATAJWA


Inaelezwa tayari mambo yameiva huko Jangwani kwani uongozi wa timu hiyo unatarajiwa kutangaza mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo baada ya mchezo dhidi ya Simba ambao utapigwa uwanja wa Taifa keshokutwa Jumapili

Ikumbukwe hivi karibuni Yanga ilimleta mtaalam kutoka Ureno ambaye atasimamia mabadiliko hayo kwa kushirikiana na Kamati ya Mabadiliko iliyoundwa na Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla

Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amewaambia Wanayanga kuwa wakae mkao wa kula kwani mambo yameiva.Akihojiwa na chombo kimoja cha habari jana, Nugaz alisema wiki ijayo watatangaza mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo
Hii ni habari njema kwa wadau wa klabu ya Yanga ambao kwa muda mredu wamekuwa na shauku ya kuona jambo hilo likitokea

Mbali na mipango hiyo ya mabadiliko ya kiuendeshwaji kuna tetesi kuwa Rostam na GSM watajwa kufanya uwekezaji ndani ya klabu hiyo mara tu mabadiliko yatakapotangazwa .

Yanga ndo klabu ya kwanza kubadili katiba yake kutambua mfumo wa uwendeshaji wa kampuni.Hata hivyo jambo hilo lilikumbana na vikwazo vingi huku mwaka juzi wakiwashuhudia watani zao Simba wakifanya mabadiliko ambayo yamewapa mafanikio makubwa

Post a Comment

0 Comments