BETI NASI UTAJIRIKE

WANACHAMA : MSOLA ATUAMBIE NINI KINAENDELEA KATI YA YANGA NA GSMWanayanga wanasubiri kusikia kauli ya Mwenyekiti wao Dk Mshindo Msolla baada ya GSM kutangaza kusitisha huduma walizokuwa wakizitoa kwa klabu ya Yanga na wakati huohuo wakibainisha kubaki na jukumu la kutengeneza na kusambaza jezi tu

Jana Yanga ilikanusha tuhuma zilizotolewa na Mwanachama Juma Magoma kuwa kuna masuala mengi ndani ya uongozi wa Dk Msolla hayaendi sawa lakini pia akatahadharisha kuwa GSM walikuwa mbioni kujiondoa kutokana na mgongano uliopo

Hili limetimia, ni wazi Wanayanga wataamini yale yaliyosemwa na Magoma kuwa yote yana ukweli kama Mwenyekiti hatajitokeza kuzungumza na kuweka mambo sawa
Lakini pia Wanayanga wanataka kusikia uongozi wake umejipangaje kuhakikisha hakuna changamoto zinajitokeza baada ya GSM kujiondoa

Inafahamika, GSM ndio waliokuwa wakilipa mishahara ya makocha wote, wachezaji lakini pia waligharamia kambi, vifaa na viwanja vya kufanyia mazoezi tangu mwezi wa kwanza
Kwa ufupi, GSM walihusika kwenye kila hatua kurejesha amani ya klabu ya Yanga tangu kuibuka lile sakata la wachezaji kuvunja mikataba kutokana na madai ya mishahara

Post a Comment

0 Comments