BETI NASI UTAJIRIKE

PASCAL WAWA "SULTAN" BADO YUPO SANA MITAA YA MSIMBAZIKiwango kilichoonyeshwa na beki mkongwe Paschal Wawa kwenye mechi za hivi karibuni, kimewashawishi mabosi wa Simba kumuongezea mkataba wa mwaka mmoja
Kwa sasa Wawa ndiye kiongozi wa safu ya ulinzi ya Simba, anatarajiwa kusaini mkataba mpya wakati wowote

Msimu huu Simba imepanga kuhuisha mapema mikataba ya nyota wake ili dirisha la usajili litakapofunguliwa wajikite katika kusaka nyota wapya
Nyota wengine ambao watasaini mikataba mipya ni pamoja na Mzamiru Yassin na Sharaff Shiboub

Taarifa za uhakika ni kuwa Simba imepanga kuongeza walinzi wawili wa kati pamoja na mlinzi wa kulia.Nyota hadi sita wanaweza kusajiliwa dirisha kubwa ambapo nafasi ya mshambuliaji mmoja pia imepewa kipaumbele

Pia viungo wawili wanaweza kutua, mmoja akiwa kiungo mkabaji.Usajili huo huenda ukawaweka matatani Tairone Da Silva na Gerson Fraga ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu

Nyota wengine ambao wanaweza wakakosa mikataba mipya ni pamoja na kiungo Said Ndemla, Yusufu Mlipili, Haruna Shamte na Shiza Kichuya aliyetua kwa mkopo usajili wa dirisha dogo

Post a Comment

0 Comments