BETI NASI UTAJIRIKE

SVEN AZUNGUMZIA FAIDA ZA LIGI KUSIMAMA NA MIPANGO YAOMkufunzi wa Simba Sven Vandenbroeck amesema mapumziko waliopewa wachezaji kutokana na janga la Corona, yatawafanya warejee wakiwa na nvguvu zaidi.Juzi Simba ilitoa mapumziko ya siku saba kwa nyota wake wa kikosi cha kwanza huku kukiwa na uwezekano muda huo kuongezwa baada ya Serikali kuzuia shughuli zote za michezo zenye mikusanyiko kwa muda wa siku 30

Sven amesema kucheza mfululizo ni changamoto iliyokuwa ikimuumiza kichwa kwani alifahamu wachezaji wake walikuwa wamechoka

"Baadhi ya wachezaji walikuwa wananiambia wamechoka kutokana na kucheza mechi mfululizo lakini kwa sasa watapata muda wa kupumzika na kurejea kwenye ubora wao," amesema Sven

"Ninaamini itakuwa bora kwetu na nafuu na itaongeza umakini katika kujihakikishia ubingwa ambao tunakaribia kuupata"

Baada ya mapumzo, ligi itakaporejea mchezo wa kwanza Simba itacheza na Ruvu Shooting
Katika michezo 10 iliyobaki, Simba inahitaji kushinda michezo mitano tu ili kujihakikishia ubingwa wa tatu mfululizo

Post a Comment

0 Comments