BETI NASI UTAJIRIKE

MWAKALEBELA AZUNGUMZIA ULIPOFIKIA MCHAKATO WA MABADILIKOMkutano Mkuu wa wanachama wa klabu ya Yanga unatarajiwa kufanyika mwezi May ikiwa ni hatua muhimu kuelekea mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji.Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema michakato mingine ya ndani inaendelea kufanyika ikisimamiwa na Kamati husika

Aidha amesema baada ya siku 30 za zuio la Serikali, wataitisha Mkutano wa Wanachama kwa ajili ya marekebisho ya Katiba ambayo yataidhina utaratibu mpya wa kusajili wanachama

Awali Yanga iliitisha Mkutano huo Februari 16 lakini haukufanyika kutokana na mkanganyiko wa kisheria kulingana na Katiba ya Yanga.Yanga imedhamiria kubadili mfumo wake wa uwendeshaji wa klabu hadi kufikia mwishoni mwa msimu huu

Hata hivyo imelenga kufuata utaratibu tofauti na ule unaotumiwa na watani zao Simba
Hivi karibuni Yanga walimleta mtaalam kutoka Ureno ambaye hata hivyo mapendekezo yake yalionekana kuwa na gharama kubwa hivyo uongozi wa Yanga pamoja na wadhamini wao GSM kuamua kuachana nayo

Kwa sasa Yanga inashirikiana na klabu moja ya La Liga ambapo mabingwa hao wa kihistoria wanajifunza mfumo wao wa uendeshaji ili kuweza kuutumia

Post a Comment

0 Comments