BETI NASI UTAJIRIKE

HIZI HAPA SABABU ZINAZOMUONDOA MOLINGA MWISHO WA MSIMU




Uongozi wa klabu ya Yanga umemuandikia barua ya kumtaka ajieleze mshambuliaji wa timu hiyo David Molinga ambaye alikacha safari ya mkoani Lindi kwenye mchezo dhidi ya Namungo Fc ambao uliamlizika kwa sare ya bao 1-1

Molinga alikuwa miongoni mwa wachezaji nane ambao hawakusafiri na timu mkoani Lindi
Inaelezwa Mcongoman huyo alichukizwa na kutopangwa mchezo dhidi ya Simba na hivyo kaamua kufanya 'mgomo baridi'

Juzi Kocha Luc Eymael alitoa malalamiko kuwa baadhi ya wachezaji wake wanachagua mechi za kucheza ambapo inadaiwa alimlenga Mcongoman huyo ambaye mara nyingi ameingia matatani kwa tabia yake ya kutopenda kukaa benchi wala kutolewa 'sub'
Yanga ilimkata Molinga kwenye usajiri wa dirisha dogo lakini kutokana na changamoto ya safu ya ushambuliaji, Eymael alipokabidhiwa timu alipendekeza arudishwe

Mwishoni mwa mwaka jana kwenye mchezo dhidi ya Biashara United, Molinga aliondoka uwanjani baada ya kocha Charles Mkwasa kumfanyia mabadiliko

Majuzi baada ya mchezo dhidi ya KMC Molinga pia aligoma kupanda basi la klabu kurejea kambini ambapo aliondoka peke yake na kutokomea kusikojulikana
Ni wazi nyota huyo aliyeifungia Yanga mabaao nane msimu huu amemkera kocha Eymael ambaye alipigania akarejeshwa kikosini

Post a Comment

0 Comments