BETI NASI UTAJIRIKE

NDEMLA KUFUATA NJIA ZA SAMATTA



Kuna uwezekano mkubwa kiungo wa Simba Said Khamis Ndemla atatimkia nchini Sweden kusakata soka la kulipwa baada ya mkataba wake na Simba kumalizika.Mwaka jana Ndemla alifanya majaribio klabu ya Ligi daraja la kwanza AFC Eskilstuna na inaelezwa alifuzu majaribio lakini klabu hiyo ikashindwa kufikia dau la usajili lililowekwa na Simba
Hata hivyo ifikapo mwezi Juni, Ndemla atakuwa mchezaji huru ambapo inaelezwa nyota huyo amegoma kusaini mkataba mpya'

Ndemla ni mmoja wa wachezaji waliodumu kwa muda mrefu kwenye kikosi cha Simba lakini hakuwa na msimu mzuri baada ya kuzidiwa na changamoto ya kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza

Post a Comment

0 Comments