BETI NASI UTAJIRIKE

MIAKA 5 YA KAPOMBE NA UBORA WAKE KWENYE LIGI



Ukizungumzia beki bora wa kulia hapa Tanzania katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, sidhani kama kuna jina litatokelezea kumzidi Shomari Kapombe
Msimu uliopita alikaa nje kwa muda mrefu kutokana na majeraha aliyoyapata wakati akiitumikia timu ya Taifa

Lakini tangu aliporejea dimbani, ameendeleza pale pale alipokuwa ameishia
Kapombe ndio injinia wa mashambulizi ya Simba upande wa kulia
Uwezo wake mkubwa wa kupanda na kushuka unamfanya awe tofauti sana na walinzi wengine wanaocheza namba yake

Mwamba huyu pia anaweza kucheza nafasi nyingine zaidi ya beki wa kulia
Wakati Simba ikinolewa na Pierre Lechantre, alipendelea zaidi kumtumia kama kiungo
Lakini pia wakati yuko Azam alikuwa akicheza beki namba 4 na 5 kabla kuhamishiwa upande wa kulia

Mkataba wake na Simba utamalizika mwezi Novemba mwaka huu lakini uongozi wa Simba uko mbioni kumpa mkataba wa muda mrefu ili aendelee kubaki Msimbazi

Post a Comment

0 Comments