BETI NASI UTAJIRIKE

KAGERE KUKUMBWA NA RUNGU LA TFF,HOFU KUKOSA KIATU CHA UFUNGAJI BORA YATAJWARais wa TFF Wallace Karia ametoa tamko kuwa wachezaji na wafanyakazi wa kigeni waliosafiri kurudi makwao, hawataruhusiwa kurejea nchini kutokana na mlipuko wa ugonjwa Corona

Karia alikwenda mbali zaidi kwa kusema wachezaji hao pia watakaporejea hawataruhusiwa kushiriki ligi.Tamko hilo limepokewa kwa mshangao na wadau wengi wa soka nchini kwani bado Serikali haijazuia watu kusafiri

Lakini pia Serikali haijafunga mipaka kuzuia wageni kuingia hivyo tamko hilo ni kama limetolewa wakati usio wake.Serikali imechukua hatua njema kuzuia michezo kwa muda wa siku 30 lakini bado haijaona kwa sasa kama kuna ulazima wa kuzuia wageni kuingia nchini, huo sio wajibu wa TFF

Jana Simba ilimruhusu mshambuliaji wake Meddie Kagere kurejea kwao Rwanda kumuona mama yake mzazi ambaye ni mgonjwa.Hili jambo la dharura na bila shaka nyota huyo alichukua tahadhari zote kabla ya kuondoka na hakuna shaka atafanya hivyo wakati atakapokuwa akirejea

Meddie Kagere atakuwa na wakati mbaya zaidi kwani kukosekana kwake ligi kuu kutamfanya ashindwe kuvunja rekodi yake kwa kufunga mabao 24 ndani ya VPL wakati huo huo akakosa kiatu mbali na kwamba anamagoli 19 na mpinzani wake Lusajo ana mabao 11 huku akiwa na advantage ya michezo  10.

Kama hatakuwa na tatizo lolote atakaporejea na Serikali ikiwa haijafunga mipaka, TFF haitakuwa na sababu ya kumzuia asicheze

Post a Comment

0 Comments