Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael alitoa mapendekezo wachezaji waliokosa safari ya mkoani Lindi wajieleze kwa nini wasichukuliwe hatua za kinidhamu.Ni mapendekezo ambayo yalibarikiwa na uongozi wa Yanga kwenye kikao walichokutana na Mbelgiji huyo hivi karibuni
Nyota takribani saba wakiongozwa na David Molinga, waliingia kwenye mtego huo wa kutakiwa kutoa maelezo.Kelvin Yondani, Lamine Moro, Erick Kabamba, Haruna Niyonzima, Mohammed Issa 'Banka' na Abdulaziz Makame 'Bui' ni miongoni mwa waliokosa safari hiyo
Yondani aweka ngumu
Wakati wachezaji wengine wakiwasilisha utetezi wao Makao Makuu, imeelezwa mkongwe Kelvin Yondani amegoma zoezi hilo
Yondani amesema yeye aliomba ruhusa mapema kuwa alikabiliwa na matatizo ya kifamilia na uongozi ulimkubalia.Hivyo hakubaliani na suala la kutakiwa kujieleza tena wakati taarifa yake iko Makao Makuu
0 Comments