BETI NASI UTAJIRIKE

CHAMA AFUNGUKA KUHUSU MKATABA MPYA NDANI YA SIMBAKiungo fundi wa Simba Clatous Chama amesema amekwenda Zambia kwa ruhusa ya uongozi baada ya kuibuka kwa virusi vvya Corona nchini lakini atakaporejea atakamilisha mazungumzo ya mkataba mpya yaliyokuwa yameanza

Hivi karibuni kuliibuka tetesi kuwa Chama aligomea mazungumzo ya mkataba mpya mpaka akiomba zoezi hilo lifanyike baada ya msimu kumalizikaChama amekanusha taarifa hizo na kusisitiza kuwa atakaporejea kila kitu kitakuwa sawa

"Kwa sasa niko mapumziko Zambia nikijikinga na janga la Corona lakini kwa ufupi tu hakuna ukweli wowote kuwa nimekataa kusaini mkataba mpya Simba, hayo ni maneno ya watu tu
"Ninachoweza kuwaambia msubiri muda sahihi utakapofika, kwani sasa nipo mapumziko nikijifua ili kulinda kiwango changu," alibainisha Chama

Msimu huu Simba imebadili utaratibu wake ambapo imeanza kuwapa mikataba mapema wachezaji wote ambao wamependekezwa na Mwalimu kuendelea kubaki Msimbazi
Nyota mwingine anayetarajiwa kupewa mkataba ni winga Deo Kanda ambaye hata hivyo anawaniwa na klabu yake ya TP Mazembe iliyomtoa kwa mkopo Simba
Mkataba wake na Mazembe unamalizika mwezi Juni

Post a Comment

0 Comments