BETI NASI UTAJIRIKE

UJANJA ANAOTUMIA CHAMA KUTIMKA MSIMBAZI



Inaelezwa uongozi wa klabu ya Simba unaendelea na mchakato wa kuwaongezea mikataba nyota wao ambao mikataba imebaki muda mfupi.Huu ni utaratibu amao mabingwa hao wa nchi wamekuja nao ili ifikapo mwezi Juni washughulikie masuala ya wachezaj wapya tu
Kiungo Mzambia Clatous Chotta Chama 'Mwamba wa Lusaka' ni miongoni mwa wachezaji ambao wako kwenye mpango wa kupewa mikataba mipya

Lakini nyota huyo kinara wa pasi za mabao ligi kuu amegomea mazungumzo ya mkataba mpya wakati huu akitaka yote yafanyike mwishoni mwa msimu.Ifikapo mwezi Julai mkataba wake utakuwa umemalizika na pengine Simba inaweza kukutana na changamoto ya kumbakisha Msimbazi

Wakati huu ambao ligi imesimama kutokana na janga la Corona, Chama aliruhusiwa kurudi kwao Zambia kushughulikia masuala binfasi

Msimu uliopita Simba ilimpoteza mshambuliaji wake kinara Emmanuel Okwi ambaye aligoma kusaini mkataba mpya akitaka mazungumzo yafanyike baada ya michuano ya AFCON kumalizika.Hata hivyo baadae akatimkia klabu ya Ittihad ya Misri

Post a Comment

0 Comments