BETI NASI UTAJIRIKE

FEI TOTO BADO YUPO SANA TU MITAA YA JANGWANI


Wakati uongozi wa Yanga kwa kushirikiana na wadhamini wao kampuni ya GSM wakiendelea kuhuisha mikataba inayoelekea ukingoni kwa nyota waliopendekezwa na kocha Luc Eymael, kiungo Feisal Salum bado ana mkataba wa muda mrefu

Feisal ni mmoja wa wachezaji ambaye iliripotiwa kuwa mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu

Mhandishi Hersi Said ambaye ni Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM lakini pia akiwa Mjumbe wa kamati ya Utendaji ya Yanga, amesema mkataba wa Feisal bado haujamalizika
Aidha, Hersi amewahakikishia Wanachama na Mashabiki wa Yanga kuwa wamejipanga kujenga kikosi imara, hivyo hawatakuwa na masihara kwenye usajili wa nyota watakaoitumikia Yanga msimu ujao

Imeelezwa Feisal alisaini mkataba wa miaka mitatu wakati akijiunga na Yanga mwaka 2018, hivyo mkataba wake utamalizika mwaka 2021

Post a Comment

0 Comments