BETI NASI UTAJIRIKE

UKIWA NA MORRISON NA MAKAMBO UNAKOSAJE UBINGWAPamoja na kuwa msimu huu Yanga ilikuwa imeweka malengo ya kuwania ubingwa, lakini mambo yamekwenda kinyume changamoto kubwa ikitokana na makosa yaliyofanyika mwanzo wa msimu hasa usajili uliofanywa na Mwinyi Zahera

Sasa mpango ulivyo ni kuwa kikosi cha maagamizi kwa ajili ya msimu ujao kinaanza kuandaliwa mapema tu, shukrani kwa wadhamini GSM ambao wameendelea kufanya mambo kwa vitendo

Tayari mkali Bernard Morrison ameongezwa mkataba wa miaka miwili, na zoezi hilo linaendelea kwa nyota wengine ambao mikataba yao imemalizika na kocha Luc Eymael amependekeza kuendelea kubaki nao

Mwezi Juni kunaweza kukawa na suprise kwani mshambuliaji Heritier Makambo anaweza kurejea Yanga

Chanzo ndani ya uongozi wa Yanga kimebainisha kuwa tayari mazungumzo na Horoya AC yameanza kuangalia uwezekano wa kumrudisha Makambo hata kwa mkopo
Wanayanga wametakiwa kuendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na GSM na kikubwa zaidi kununua jezi origino pamoja na bidhaa mbalimbali za kampuni hiyo
Kwani kwa kufanya hivyo, unakuwa umechangia juhudi zinazofanywa kuirudisha Yanga mahali pake

Post a Comment

0 Comments