BETI NASI UTAJIRIKE

KWA MARA NYINGINE MKUDE AINGIA MITINI KAMBI YA TAIFA STARSKiungo fundi wa Simba Jonas Mkude hakuingia kambini na timu ya Taifa iliyokuwa ikijiandaa na michuano ya CHAN, kambi ambayo ilivunjwa juzi baada ya michuano hiyo kuahirishwa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Corona

Kukosekana kwake Stars kuliibua mjadala mkali siku chache zilizopita hasa ikizingatiwa Mkude ni mmoja wa wachezaji wa kutegemewa kwenye timu ya Taifa
Kocha Mkuu wa Stars Etienne Ndayiragije alidai kutokuwa na taarifa za Mkude nao viongozi wa TFF wakisema hivyo

Sasa wakala wa kiungo huyo Juma Ndambile amefunguka kuwa nahodha huyo wa zamani wa Simba ana mambo yanayomkwaza na hajisikii furaha kuitumikia timu ya Taifa
Aidha Ndambile amesema Mkude yuko tayari kuyaweka bayana masuala hayo kwa uongozi wake wa Simba pamoja na TFF

Kuna uwezekano Mkude atatangaza kustaafu kuitumikia timu ya Taifa kama ilivyokuwa kwa Shomari Kapombe ambaye amerejea Stars hivi karibuni ikiwa ni zaidi ya miezi nane imepita tangu alipotangaza kustaafu kutumikia Stars kwa muda

Iliwahi kuripotiwa nyuma kuwa Mkude alikuwa na mvutano na TFF kuhusu madai mbalimbali aliyokuwa nayo kwa Shirikisho hilo

Post a Comment

0 Comments