BETI NASI UTAJIRIKE

SVEN AJIANDAA KUPEWA MKATABA MPYA SIMBAKocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck huenda akaongezwa mkataba mpya mwishoni mwa msimu pale mkataba wake utakapokuwa umemalizika.Sven alitua Simba mwezi Disemba 2019 kwa mkataba wa miezi sita ambao utamuweka Msimbazi mpaka mwishoni mwa msimu

Mbelgiji huyo anaelekea kutimiza malengo aliyopewa ambayo ni kutwaa ubingwa Ligi Kuu huku pia akiwa na nafasi ya kutwaa kombe la FA Simba ikifanikiwa kutinga robo fainali
Baada ya kujihakikishia ubingwa hesabu zimeelekezwa michuano ya Ligi ya mabingwa barani Afrika Simba ikitarajiwa kuwa timu pekee itakayoshiriki kwa upande wa Tanzania baada ya alama kutotosha kuendelea kupewa nafasi mbili na CAF

Mwishoni mwa msimu uongozi wa Simba unatarajiwa kufanya tathmini kabla ya maamuzi ya kumuongeza mkataba kufikiwa


Post a Comment

0 Comments