BETI NASI UTAJIRIKE

SIMBA YAVUNJA NA KUWEKA REKODI MPYA LIGI KUU


Ushindi wa mabao 8-0 hidi ya Singida United unaifanya Simba iweke rekodi ya kufunga mabao saba au zaidi kwenye ligi katika mchezo mmoja kwa misimu mitatu mfululizo
Msimu wa 2017/18 Simba iliifumua Ruvu Shooting mabao 7-0 kisha msimu uliopita wakapata ushindi wa mabao 8-1 dhidi ya Coastal Union

Hapo jana  wamerudia rekodi ya mabao 8 dhidi ya Singida United
Simba imeendelea kuweka rekodi ya kuwa timu inayofunga mabao mengi kwa msimu huku Meddie Kagere akikaribia kuivunja rekodi yake ya mabao ya msimu uliopita
Kagere anahitaji kufunga mabao matano tu kwenye michezo 10 iliyobaki ili kuvunja rekodi yake ya mabao 23 ya msimu uliopita

Ni suala la muda tu Simba itatangaza ubingwa kwa msimu wa tatu mfululizo

Post a Comment

0 Comments