Kikosi cha Yanga leo kinashuka uwanja wa Taifa kuikabili Mbao Fc katika mchezo ambao utapigwa saa moja usiku.Huo ni mchezo wa 24 kwa Yanga wakati kwa upande wa Mbao Fc ni mchezo wa 26
Baada ya kushinda mechi zote mbili zilizopita, Yanga itakuwa ikisaka ushindi wa tatu mfululizo.Muhimu zaidi mabingwa hao wa kihistoria watatumia mchezo huu kama sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumapili ijayo
Kikosi atakachotumia Eymael leo kitatoa mwanga wa kikosi kitakachoshuka dimbani March 08.Viingilio vya mchezo huo VVIP ni Tsh 15,000/-, VIP B na C ni Tsh 10,000/- wakati upande wa mzunguuko ni Tsh 5,000/-Lakini kwa wale watakaonunua jezi orojino za Yanga kwa bei ya Tsh 35,000/-, watapatiwa tiketi za bure
0 Comments