Beki kisiki wa Yanga mkongwe Kelvin Yondani ni mmoja wa wachezaji ambao hata pale atakapostaafu ataacha alama kwa soka la Tanzania.Yondani alisajiliwa na Simba mwaka 2006 akitoka klabu ya Mwanza United ya jijini Mwanza
Mwaka 2012 aliikacha Simba na kujiunga na Yanga, klabu anayoitumikia mpaka sasa
Ana takribani miaka 14 au zaidi anacheza soka la ushindani lakini bado yuko imara kuliko walinzi wengi wadogo
Yondani amesema siri ya kudumu kwa muda mrefu ni pamoja na kufanya mazoezi, kula chakula kizuri na kujipa muda mrefu wa kupumzika.Mkongwe huyo amefunguka kuwa wachezaji wengi wa sasa wanaendekeza sana starehe na ndio maana ni nadra kuwaona wakin'gara kwa muda mrefu
"Mimi nafanya sana mazoezi, lakini pia nakula vizuri. Usiku napata muda mrefu wa kupumzika..hayo mambo ya kujirusha hasa usiku huwa siyapi nafasi," amesema Yondani
"Nawashauri vijana wazingatie hayo, waache kupoteza muda mwingi kwenye kuchat na kujirusha usiku, wazingatie misingi sahihi ili walinde viwango vyao"
Yondani yuko ukingoni kwenye mkataba wake na klabu ya Yanga lakini huenda akaongezwa mwaka zaidi ili aendelee kubaki Jangwani
0 Comments