BETI NASI UTAJIRIKE

NCHIMBI ATUMA SALAMU ZA VITISHO KWA WAPINZANI WA YANGA WAKIWEMO SIMBA


Baada ya juzi kufunga mabao mawili kwenye mchezo dhidi ya Alliance Fc, mshambuliaji wa Yanga Ditram Nchimbi amesema atahakikisha anafunga mabao mengi zaidi katika michezo iliyobaki
Kabla ya mabao yake ya juzi, Nchimbi hakuwa ameifungia Yanga tangu alipojiunga nayo mwezi Januari 2020
Hata hivyo changamoto hiyo inaweza kuwa ilichangiwa na uamuzi wa kocha Luc Eymael kumbadilishia majukumu na kumtumia nafasi ya winga
Juzi alimrudisha nafasi ya mshambuliaji wa kati na hakufanya makosa kwani dakika 45 za kipindi cha pili alizopewa zilimtosha kuihakikishia Yanga ushindi muhimu

"Nimesajiliwa Yanga kwa ajili ya kufunga mabao licha ya kwamba nacheza na ninaweza nikafanya majukumu mengine makubwa, watu wanataka kuona nazitikisa nyavu, hilo linanifanya nipambane kwa kadri ninavyoweza ili kutimiza malengo yangu. Hakuna mshambuliaji asiyependa kuwa na mabao mengi, binafsi natamani uwepo wangu utambulike kwa wadau wa soka kwa kuzitikisa nyavu, sijakata tamaa nitapambana niwezavyo, naamini nitafunga sana tu kwa mechi zilizosalia"

Post a Comment

0 Comments