BETI NASI UTAJIRIKE

MANARA AMKARIBISHA TSHISHIMBI NDANI YA SIMBA , KAULI YAKE YAIBUA MASWALI



Afisa Habari na Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amesema anatamani siku moja kumuona nahodha wa Yanga Papy Tshishimbi akivalia uzi wa klabu ya Simba
Manara ametoa kauli hiyo siku moja tu baada ya Tshishimbi kugoma kuongeza mkataba huko Yanga

Nyota huyo kutoka DRC mkataba wake na Yanga unamalizika mwezi wa nane

"Box 2 Box Midfielder Papy Tshishimbi siyo siri mimi nnamshabikia kinoma. Nikiulizwa natamani siku moja aje kucheza Simba. Yes napenda iwe hvyo ila kwa sasa bado ni mchezaji wa Gongowazi. But u never know ya kesho," ameandika Manara kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram

Zipo taarifa za chinichini kuwa Simba inataka kumsajili Tshishimbi achukue nafasi ya Gerson Fraga ambaye huenda asipewe mkataba mpya

Post a Comment

0 Comments