Mabingwa wa kihistoria Tanzania, Yanga kesho Jumamosi watakuwa dimba la Uhuru kupepetana na Alliance Fc katika mchezo wa ligi kuu
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amethibitisha kuwa mchezo huo utapigwa uwanja wa Uhuru kwa kuwa matengenezo yanaendelea uwanja wa Taifa
Aidha Bumbuli amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo huo kama walivyofanya mchezo uliopita dhidi ya Gwambina FC
Mbio za ubingwa bado
Katika hatua nyingine Bumbuli amesema Yanga bado iko kwenye mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu
"Tunawaambia mashabiki wetu waendelee kutuunga mkono, bado hatujakata tamaa kuwania ubingwa wa VPL"
"Hatma yetu kwenye ubingwa itafahamika baada ya kuwa tumecheza mechi zetu 16 na zile mbili za viporo," amesema
0 Comments