BETI NASI UTAJIRIKE

TSHISHIMBI ATOA SABABU ZA KUPOTEZA POINTI MCHEZO DHIDI YA POLISI TANZANIA

Nahodha wa Yanga Papy Tshishimbi amesema mazingira ya uwanja wa Ushirika yamechangia wao kushindwa kuondoka na alama zote tatu kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Polisi Tanzania


Yanga ilitangulia kufunga bao la kuongoza kwenye mchezo huo kupitia kwa Tariq Seif aliyeunganisha kwa kichwa pasi murua ya Bernard Morrison
Hata hivyo Polisi Tanzania walisawazisha bao hilo kwenye dakika ya 70 kupitia kwa Sixtus Sabilo

Tshishimbi amesema mazingira ya uwanja yaliwapa wakati mgumu hasa kwenye kipindi cha pili dhidi ya wenyeji wao Polisi ambao walionekana kuuzoea

"Tulipata bao la kuongoza na tulifurahi mwisho wa siku takashindwa kulinda bao letu kutokana na ugumu wa eneo la kuchezea kwani mpira ulikuwa hautulii," amesema
"Wao walikuwa ni wenyeji na wanautambua vizuri uwanja wakatumia nafasi hiyo kushinda, tunashukuru kwa kuwa tumemaliza salama mchezo ni mwendelezo wetu kujipanga kwa jili ya mechi zinazofuata"

Baada ya mchezo huo Yanga itaelekea mkoani Tanga kuifuata Coastal Union kwa ajili ya mchezo mwingine ambao utapigwa Jumapili, Februari 23

Post a Comment

0 Comments