BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMATATU TAREHE 03-02-2020


Raisi wa Atletico Madrid Enrique Cerezo amedai kuwa klabu hiyo "isingekubali kutapeliwa" baada ya kushindikana usajili wa streka wa Paris St-Germain na Uruguay Edinson Cavani. (ESPN)
Mshambuliaji wa Chelsea na England Tammy Abraham amesikitishwa na klabu yake kushindwa kumsajili Cavani. (Mirror)
Timu inayomilikiwa na mchezaji nyota wa zamani wa Manchester United David Beckham, Inter Miami iliyopo Marekani inataka kuoneza nguvu ya kumsajili Cavani pale mkataba wake na PSG utakapofika tamati mwishoni mwa msimu. (L'Equipe)
Wakala wa Cavani angelikataa kujiunga na Chelsea na Manchester United bila kujali ukubwa wa ofa kutoka kwenye klabu hizo. (Mirror)
WillianHaki miliki ya picha
Winga raia wa Brazil Willian, 31, angependelea kusaini mkataba mpya utakaombakiza Chelsea kuliko kujiunga na mabingwa wa Uhispania Barcelona. (ESPN)
Barcelona wametupilia mbali ofa ya kumsajili mshambuliaji wa Napoli Fernando Llorente, 34. (AS)
Meneja wa Chelsea Frank Lampard anataka kusajili kipa mpya baada ya kuporomoka kiwango cha kipa Kepa Arrizabalaga, 25. (Express)
Kiungo Mesut Ozil, 31, alipewa nafasi ya kuihama Arsenal mwezi uliopita na kocha wake Mikel Arteta alikuwa tayari kumruhusu. (Mirror)
OzilHaki miliki ya picha
Kiungo wa Lille Boubakary Soumare, 20, almekataa ofa nono ya kujiunga na klabu ya Newcastle mwezi Januari akiamini kuwa anaweza kujiunga na Liverpool ama Manchester United mwishoni mwa msimu. (Le10sport - in French)
Liverpool wanajipanga kumsajili mshambuliaji kinda na machachari wa Borussia Dortmund na England, Jadon Sancho, 19, mwishoni mwa msimu. (Express)
GiroudImage capt
Kocha wa Lazio Simone Inzaghi amesema laiti angelimpata mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Olivier Giroud, 33, kungewezesha ndoto zake za kufukuzia ubingwa kuwa na "machaguo zaidi." (Gazzetta)
Kocha Roy Hodgson ameionya bodi ya Crystal Palace kuwa watakuwa na kazi ngumu ya kuboresha kikosi chao mwishoni mwa msimu. (Standard)
Hodgson, ambaye anamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu anaitaka klabu hiyo kufikiria namna bora ya kuendelea nayo baada ya kushindwa kufurukuta kwenye dirisha la usajili la mwezi uliopita. (Telegraph)

Post a Comment

0 Comments